- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) imeipongeza Halmashauri ya Manispaa Ya Shinyanga katika utekelezaji mzuri wa shughuli za usafi wa mazingira.
Akizungumza wakati wa kukabidhi tuzo Meneja wa Mradi wa usafi wa mazingira Ndg .Olivier Germain alisema kuwa Manispaa ya Shinyanga imekuwa na mchango mkubwa sana katika kufanikisha shughuli nzima za utekelezaji wa usafi na Mazingira mpaka Shirika la Maendeleo (SNV) wakatambua, wakathamini mchango na kuamua kutoa tuzo hii ambayo leo imekabidhiwa rasmi kwa Mkurugenzi wa Manispaa Mwl. Alexius Kagunze kwa niaba ya Manispaa kwa ujumla.
“Manispaa ya shinyanga hakika tunatambua na kuthamini mchango wenu katika kutekeleza vizuri mradi huu wa usafi wa mazingira hakika mnastahili kupewa tuzo “alisema Olivier
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa Mwl. Kagunze alisema amepokea kwa mikono miwili huku akiwashukuru sana SNV kwa tuzo hii na pia aliwapongeza kwa kuamua kuichagua Manispaa ya Shinyanga kuwa sehemu ya kufanya shughuli za utekelezaji wa usafi wa mazingira kwani wangeweza kufanyia Halmashauri nyingine yoyote lakini waliamua iwe hapa jambo ambalo Manispaa inalipokea kama ni heshima kubwa sana.
"Kwa niaba ya Mstahiki Meya Mhe. Elias Masumbuko, Baraza la Madiwani Menejimenti na Watumishi wote wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tunapokea kwa mikono miwili Tuzo, tunawashukuru sana ninyi SNV kwa kutambua na kuthamini uwepo wetu na tunawapongeza sana kuchagua Manispaa kwetu kama sehemu ya utekelezaji wa shughuli za usafi wa Mazingira na tunawakaribisha sana wakati mwingine kwa jambo lolote Manispaa itawapatia ushirikiano wakati wote," alisema Mwl Kagunze
Ikimbukwe shirika la maendeleo la uholanzi (SNV) linashughulika na usafi wa mazingira ambapo kwa Tanzania shirika hili linaendesha shughuli zake katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Jiji la arusha, shughuli ambazo wameweza kuzifanya katika Manispaa ya Shinyanga kwa kipindi cha miaka mitano ni Ujenzi wa Vyoo vya kisasa katika stendi ya Wilaya na Mkoa , Ujenzi wa mtambo wa kuchakata tope kinyesi uliopo kizumbi pamoja ununuzi wa mtambo wa kunyonya tope kinyesi kutoka Africa Kusini na miradi mengine zaidi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga