- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Manispaa ya Shinyanga imefanya uchaguzi wa Meya ambapo Mh Elias Ramadhani Masumbuko (Diwani Kata ya Chamaguha Amepita kwa Kishindo kwa katika Uchaguzi huo Akipata Kura zote za Ndio hivyo akipita kwa Asilimia zote na Kumfanya kuwa Mshindi kwenye Uchaguzi huo.
Uchaguzi huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Manispaa na kuhudhuriwa na Baraza la Madiwani la Manispaa, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, Katibu tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg Jomaary Mrisho Satura,Wakuu wa Taasisi Mbalimbali, Watumishi, wakuu wa idara na vitengo pamoja na Wananchi.
Akitoa neno la shukrani baada ya kuchaguliwa Mstahiki Meya Mh Elias Ramadhani Masumbuko aliwashukuru wajumbe kwa imani waliyoonesha kwake na kuahidi kuwalipa utumishi uliotukuka.
“Nawaomba Waheshimiwa Madiwani wenzangu mfahamu kuwa tuna kazi kubwa mbele yetu kuhakikisha Halmashauri yetu inapiga hatua, niwaombe ushirikiano ili kufikia malengo yetu yaliyoainishwa vizuri kwenye ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi”. Alisema Mh Elias Ramadhani Masumbuko
Kwa upande wa watumishi Mh Elias Ramadhani Masumbuko amewataka kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ubunifu ili kuleta tija katika huduma mbalimbali za Wananchi.
Zoezi la kupiga Kura likiendelea
Mhe Diwani Akipiga Kura
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Ndg Jomaary Mrisho Satura
Mh Mstahiki Meya Upande wa Kulia Katika Picha ya Pamoja na Naibu Meya
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga