- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
HALMASHAURI ya Manispaa ya Shihyanga Februari 10, 2023 imekabidhi Pikipiki 8 Maafisa Afya pamoja na Vyeti kwa Watendaji wa Kata zote 17 ikiwa ni sehemu ya kutambua jitihada zao katika utendaji kazi, jambo ambalo lilipelekea Manispaa kuibuka Mshindi wa Kwanza kwa Usafi Kitaifa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Pikipiki na vyeti hivyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mh. Elias R. Masumbuko alisema kuwa, kukabidhiwa kwa pikipiki hizo kutawawezesha kufanya kazi kwa tija zaidi ili kuendelea kuifanya Manispaa ya Shinyanga kuwa kinara wa Usafi Kitaifa.
"Baraza la Waheshimiwa Madiwani, Menejimenti na Watumishi wote wa Manispaa wametambua na kuthamini kazi zenu na ndiyo maana kwa kauli moja walikubaliana mpatiwe pikipiki hizi maafiisa Afya 8 na Vyeti kwa Watendaji wa Kata zote 17 ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wenu katika kuipatia ushindi wa Usafi Manispaa ya Shinyanga," alisema Mh. Masumbuko.
Awali akimkaribisha kukabidhi Pikipiki hizo Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Ndg. Jomaary M. Satura alisema kuwa, Maafisa Afya Mazingira na Watendaji wa Kata zote wamefanya kazi kubwa sana na kujituma jambo ambalo lilipelekea Ushindi wa Kitaifa kwa kuibuka namba moja kwenye Usafi.
"Hivyo basi, Manispaa ya Shinyanga itaendelea kuwatambua na kuwawezesha watumishi wake wote katika ili na wao waweze kuboresha utendaji kazi kuongeza tija katika shughuri zao za kila siku, lakini pia nitoe angalizo kwa watumishi wote kuacha kufanya kazi kwa mazoe jambo ambalo mara nyingi limekuwa likipelekea baadhi yenu kuanza kuharibu kazi zenu, badala yake kuweni wabunifu zaidi kila siku", Satura alisisitiza.
Kukabidhiwa kwa Pikipiki hizo ni muendelezo wa juhudi za Manispaa ya Shinyanga kutambua na kuthamini kazi za watumishi wake ikiwa ni moja kati ya mikakati yake itakayowapelekea watumishi kuendelea kuwa wabunifu, jambo ambalo lilipelekea Manispaa kupata Tuzo mbalimbali Kitaifa.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga