- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Disemba 20,2024 imekabidhi Mikopo ya asilimia 10 yenye thamani ya shilingi Milioni 90,000,000 itokanayo na mapato ya ndani ya Halmashauri kwenye vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu
Akikabidhi hundi ya mikopo hiyo Mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko amevitaka vikundi hivyo kuwa na nidhamu ya pesa pamoja na matumizi sahihi kulingana na andiko la miradi yao.
“Serikali inatoa mikopo hii kwa lengo la kupunguza wimbi kubwa la vijana wasio na ajira, kuweni na nidhamu na fedha hizi, kama ambavyo maandiko yenu ya miradi yameonyesha ndivyo hivyo fedha hizi zikatumike na fedha hizi zisiwe chanzo cha matatizio na migogoro. Amesema Mhe. Masumbuko
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Elisha Robert ambaye amemuwakilisha mkurugenzi wa manispaa Mwl. Alexius Kagunze amesema halmashauri itaendelea kutoa fedha kwa vikundi vyote vitakavyokidhi taratibu zote kama maelekezo ya serikali yanavyohitaji.
Naye Bi.Salome Komba ambaye amemuwakilisha Ndg. Peres Kamugisha Mkuu wa divisheni ya Maendeleo ya jamii Manispaa amesema jumla ya vikundi vitatu vimepatiwa mikopo, kikundi cha VIJANA SEAT COVER kutoka kata ya Kambarage ambacho kimepatiwa mkopo wa Shilingi 50,000,000/= kikundi cha FIVE MAMA’S cha wanawake kutoka kata ya Ngokolo, Tsh 20,000,000/= pamoja na Mtu mmoja mwenye ulemavu kutoka kata ya Ndala kiasi cha Tsh 20,000,000/= kwa ajili ya duka la vifaa vya ujenzi, ambapo mikopo hiiyo imetolewa chini ya Sura ya 290 na kanuni zake chini ya kifungu cha 37A (4) zinazojulikana kama kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo kwa vikundi vya Wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga