- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga laadhimia kutenga siku maalumu kwa ajili ya kufanya usafi wa mazingira kwa wakazi wote wa manispaa ya shinyanga ili Kuhakikisha mji unaendelea kuwa kwenye hadhi yake,ili iendelee kushika na kutetea Tuzo ya usafi wa mazingira ambayo hutolewa na wizara ya afya kwa Mwaka wa tatu mfululizo.
Haya yamebainishwa Leo Februari 07, 2025 na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Ndg. Revocatus Lutunda wakati akijibu swali alilohoji Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Kizumbi Ndg. Reuben Kitinya juu ya mkakati wa manispaa Katika Kuimarisha usafi wa mazingira.
“Katika Kuhakikisha hadhi ya usafi mazingira kwa manispaa yetu inaendelea, tumejipanga kuandaa siku maalumu kwa mwezi huu, kutenga siku maalumu kwa ajili ya kufanya usafi kwa wakazi wote wa halmashauri hii ili tuweze kuendelea Kuhakikisha halmashauri yetu inaendelea kuwa safi, na kutetea tunzo yetu tuliyoshinda kwa msimu wa tatu mfululizo”. Amesema Ndg. Lutunda
Katika hatua nyingine Baraza la Madiwani limewapongeza, maafisa elimu shule ya msingi na sekondari kwa kufanya vizuri Katika mitihani ya upimaji wa kitaifa darasa la saba, kidato cha pili na kidato cha nne ambapo manispaa ya shinyanga Katika matokeo ya darasa la saba imekuwa ya kwanza kimkoa kwa ufaulu wa 88.4%. kitaifa imekuwa ya 46 kati ya halmashauri 184.katika kidato cha pili kwa ufaulu wa 87%. Huku kidato cha nne wanafunzi wamefaulu kwa 97% na kuifanya manispaa ya shinyanga kushika nafasi ya kwanza kimkoa kati ya halmashauri sita za mkoa huu.
Mkutano wa Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga leo umeketi kupokea na kujadili taarifa kutoka kwenye kamati za kudumu za Halmashauri, taasisi mbalimbali za Serikali (SHUWASA, TARURA na TANESCO) zinazofanya kazi ndani ya Manispaa ya Shinyanga kwa kipindi cha robo ya pili ya (Oktoba-Disemba) kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga