- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na George Mganga, SHY MC
HALMASHAURI ya Manispaa ya Shinyanga imegawa sehemu ya Vishikwambi (TABLETS) 549 kwa walimu wa Shule za Msingi na Sekondari zilizopo ndani ya Manispaa ya Shinyanga.
Zoezi hilo limefanyika Januari 24, 2023 katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga ambapo jumla ya Vishikwambi 257 viligawiwa kwa Walimu wa Shule za Msingi na 292 wakipewa kwa Walimu wa Sekondari.
Ugawaji wa Vishikwambi hivyo umefanyika kutokana na maagizo ya Serikali ili kuwawezesha Walimu kuendana na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambayo itasaidia katika michakato ya ufundishaji na kuwasilisha Elimu kwa Wanafunzi.
Huu ni muendelezo wa utoaji wa Vishikwambi hivyo ambapo awali viligawiwa katika awamu ya kwanza Vishikwambi 470 ambavyo pia tayari vimeshaanza kutumika mashuleni kama ilivyo maelekezo ya Serikali.
Awali akikabidhi vishikwambi hivyo Mwl. Tuzo Mpwaga ambaye ni Afisa Elimu Vifaa na Takwimu wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, alisema kuwa kutolewa kwa Vishikwamhi hivyo kwa walimu ni utekelezaji wa maelekezo ya Serikali kuwa wapatiwe waalimu viende kuwasaidia katika utekelezajj wa majukumu yao ya kila siku katika kazi zao.
"Vishikwamhi hivi viende kutumika kwa maslahi mapana ya kazi na majukumu yenu na wala siyo vinginevyo, na kwakuwa Serilikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayo nia njema kwenu, nanyi tunaimani mnakwenda kutekeleza maelekezo ya Serikali yake ambayo imetoa kwa nia njema kabisa kwenu", alisema Mwl Mpwaga.
Utoaji wa Vishikwambi kwa walimu wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambao unaendelea mpaka sasa, ni utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ambapo Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa alisisitiza ugawaji Vishikwambi kwa walimu ufanyike kwa haraka ili waendelee na uboreshaji wa utoaji huduma kwa walimu.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga