- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imeendesha mafunzo wa ya mfumo wa MSHITIRI (mjaziaji bidhaa za afya zilizopungua kutoka Bohari ya Dawa Taifa - MSD) kwa Waganga Wafawidhi wa Hospitali, Vituo vya Afya, Zahanati na watunza Stoo za Dawa wote kwa lengo la kuwezesha ili waweze kusimamia, usambazaji na udhibiti mzuri wa dawa katika maeneo yao ya kiutendaji.
Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Ndg. Jomaary Mrisho Satura aliwaeleza wataalamu hao kuwa Serikali inayo dhamira njema sana kwa wataalamu na wananchi wote kwa ujumla ndiyo maana ikaamua kuja na mfumo huu ambao ukitekelezwa kwa umakini na uzalendo mkubwa itaweza kuisadia Serikali kuondoa urasimu, ufujaji na hivyo wananchi watanufainka na mfumo huu kama lengo la Serikali lilivyo.
"Serikali imeamua kuboresha eneo hili la utoaji wa dawa kwenu wataalamu na mawakala ili kuweza kutoa huduma kwa urahisi na kwa wakati, kuondoa uwezekano wa msimamizi au wakala kuingia matatizoni, kuondoa urasimu ambao awali ulikuwepo kwakuwa hivi sasa ataomba kupitia mfumo, na mwisho kabisa lengo kusidiwa la Serikali litakuwa limefikiwa kikamilifu," alisema Satura.
Awali akimkaribisha kufungua mafunzo hayo, Mtunza Stoo za Dawa Ndg. Charles Malogi alisema kwamba Manispaa ya Shinyanga inatekeleza maelekezo ya Serikali ambapo baadhi ya wataalamu walialikwa kuhudhuria mafunzo ya mfumo huo yaliyofanyika ngazi ya Mkoa ambapo walielekezwa na wao kushusha chini mafunzo hayo kwa wataalamu ambao ni Waganga Wafawidhi wa Hospitqli, Vituo vya Afya, Zahanati na watunza Stoo za Dawa wote wa Manispaa tukio ambalo ndiyo linafanyika leo tarehe 15 Machi, 2023.
Malogi aliwataka wataalamu kuupokea mfumo huu kwa mikono miwili kwakuwa unakuja na suluhisho la kudumu dhidi ya malalamiko yaliyokuwa yakitolewa awali, huku akiwataka kwenda kuutekeleza kwa uzalendo na ufanisi ili uweze kuleta matokeo chanya kwa walengwa amabo ndiyo wananchi na ndiyo walipa kodi wa Nchi hii.
"Twendeni tukautekeleze mfumo huu kwa vitendo huku tukitanguliza uzalendo na ufanisi katika kuwahudumia wananchi wetu, na ndiyo maana tupo hapa na kwamba tumemualika Mkurugenzi wa Manispaa ili aje atoe nasaha zake kenu kwakuwa naye ni sehemu ya Serikali ambaye anayo dhamana kubwa kwa Majispaa ya Shinyanga, tuupokee mfumo huu kwa mikono miwili tukautekeleze ipasavyo," alisema Malogi
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga inakeleza Mfumo huu wa MSHITIRI ambao unakwenda kuwasaidia wataalamu kusimamia AFUA mbalimbali za mfumo wa Ugavi wa Bidhaa za Afya ikiwamo kufanya Medicine Audit mara kwa mara katika vituo vya kutolea huduma kwa ajili ya kupunguza changamoto zitokanazo na usimamizi mbovu wa bidhaa za afya.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga