- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MANISPAA YA SHINYANGA YAANZA MAFUNZO ElEKEZI YA KIELETRONIKI YA MFUMO WA MUKI KWA WATUMISHI
Na. Shinyanga Mc
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo tarehe 15 Septemba, 2023 imeanza mafunzo elekezi ya kieletroniki ya mfumo wa MUKI kwa muda wa siku mbili kuanzia leo tarehe 15 mpaka 16 Septemba, 2023 kwa watumishi wa Manispaa katika ukumbi wa shule ya msingi Buhangija iliyopo katika kata ya Ibinzamata.
Akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo hayo Bi Getruda Gisema ambaye ni Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu amewaeleza washiriki wa mafunzo hayo kuwa Serikali imeleta mfumo huu ili kurahisisha kazi na kupunguza gharama za matumizi mbalimbali kwani mfumo huu niwa kidigitali hivyo matumizi makubwa ya shajala na mambo mengine havitatumika bali vitatumika zaidi kwa kutumia Vishikwambi na mpakato(laptop)ili kujengea uelewa wa urahisi kwa watumishi katika kujifunza mambo mambalimbali ya kiutumishi.
Bi Gisema ameeleza kwamba awali Serikali ilikuwa ikitoa mafunzo haya kwa watumishi mara tu wanapoajiriwa lakini yalikuwa yanatolewa kwa njia ya kawaida yani kusomewa na kuelezewa kwa mdomo mambo mbalimbali ya kiutumishi lakini kwa kutumia mfumo huu wa MUKI watumishi wanajiunga kieletroniki kwa kujaza taarifa binafsi ambapo baada ya kuingia katika mfumo huo wataweza kusoma na kujifunza mambo mbalimbali ya kiutumishi.
Sanjali na hilo Bi Gisema amewaeleza washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha kuwa wanajisajili katika mfumo huo ili kujisomea na kufanya mitihani itakayo wawezesha kupata cheti cha kuhitimu mafunzo ya kiutumishi kwa njia ya kieletroniki.
Kupitia mfumo huu wa MUKI utaenda kusaidia watumishi kuweza kujua kanuni na maadili ya kiutumishi, majukumu yao ya kitaaluma na kujua stahiki zao mbalimbali pamoja na kujifunza mambo ya kiutumishi muda wowote na mahali popote kwa njia ya kieletroniki.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga