- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wajumbe wa Kamati ya lishe Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Disemba 13, 2024 wamefanya kikao kazi kuelekea bajeti mpya 2025/2026 ambapo wajumbe hao wameafiki kuingiza mpango wa kilimo cha viazi lishe kwa shule zote za msingi na sekondari ili kujenga afya za wanafunzi.
Kikao hiki kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Lewis Kalinjuna uliopo halmashauri ya manispaa ya shinyanga ambapo wamesema ili kuondokana na udumavu , ukondefu, utapiamlo pamoja na viliba tumbo ipo haja ya kuanzisha bustani za viazi lishe na mbogamboga kwa shule zote Manispaa ya Shinyanga.
Ndg. Peres Kamugisha Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ambae amemuwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa Mwl. Alexius Kagunze amesema kuwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wanasimamiwa sana juu ya lishe bora , lakini wakiwa zaidi ya miaka mitano wanakuwa wanasahaulika haswa kipindi ambacho wanafikia umri wa kuanza darasa la awali, ipo haja basi kwa bajeti hii ya 2025/2026 kuweka bajeti ya kilimo cha bustani ya viazi lishe, mbogamboga na matunda kwenye shule zetu ili kuondokana na utapiamlo,viliba tumbo, ukondefu kwa watoto haswa waliopo shuleni.
Kwa upande wake Ndg. Pius Sayayi Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi Rasilimali watu Manispaa ya Shinyanga amesema asilimia kubwa shule zote zina maeneo ya kulima bustani za viazi lishe na mbogamboga ,hivyo ni vyema kuanzisha kilimo hicho ambacho kitasimamiwa na wataalamu wa kilimo (maafisa kilimo kata) ili wanafunzi wote wapate lishe wawapo shuleni .
Awali akizungumza kwenye kikao hichi Afisa lishe Manispaa ya Shinyanga Ndg. Amani Mwakipesile amesema Kitengo cha Lishe Manispaa ya Shinyanga kimekuwa na utaratibu wa kufanya vikao hivi kuelekea Bajeti mpya ili kuona utendaji kazi na utekelezaji wa majukumu yao kwa lengo la kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanayosababishwa na kutozingatia mlo kamili pamoja na kutozingatia makundi sita ya chakula.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga