- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imewezesha Ujenzi wa Kituo cha Afya Seseko kilichopo Kata ya Mwamalili ndani ya Mkoa wa Shinyanga.
Kupitia mapato yake ya ndani, Manispaa imeamua kuwezesha ujenzi huo rasmi mwaka jana ili kuwasaidia wananchi wa eneo hilo wenye changamoto ya kukosa huduma ya afya.
Wananchi wa Seseko walianzisha ujenzi wa kituo hicho mwaka 2002 lakini kutokana na changamoto ya kukosa fedha walishindwa kuendelea, hadi Manispaa ilipoamua kuweka mkono wake kwa ajili ya kujenga kituo hicho.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Dkt. Jomaary Satura, amesema wameamua kuisaidia Seseko kutokana na wananchi wake kukosa huduma kiasi cha kwamba kulazimika kusafiri maeneo mengine yaliyo mbali, jambo ambalo limekuwa likiwapa mtihani wagonjwa hususani wakina mama wajawazito.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Jomaary Satura akizungumzia mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Seseko.
“Tumechagua kujenga hapa sababu hakuna huduma, wananchi wapo kwa ajili yetu nasi tuna wajibu wa kuwasaidia ili kuwatengenezea mazingira mazuri ya huduma za afya”, amesema Dkt. Satura.
Aidha, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Elisha Robert Ndaki, amesema Manispaa imekuwa ikitoa fedha na sasa wameshatoa zaidi ya Tsh. Mil 35 kuwezesha ujenzi huo ambao bado unaendelea.
Kituo cha Afya Seseko namna kinavyoonekana hivi sasa baada ya Manispaa kuwezesha ujenzi wake.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga