- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na George Mganga, SHY MC
HALMASHAURI ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Ofisi ya Mkurugenzi, leo Januari 27, 2023 imeitisha Kikao Maalum na Wadau wa Shughuli za Sherehe na Burudani, ili kujadili mabadiliko ya Sheria ndogo na Maelekezo ya namna ya Ulipaji wa Ada na Ushuru unaotokana na shughuli mbalimbali za Sherehe na Burudani.
Wadau mbalimbali wa Shughuli za Sherehe na Burudani pia Watendaji wa Kata waliojitokeza katika kikao.
Akimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni, Vijana na Michezo, Charles Luchagula, amesema lengo mahususi la kuitishwa kwa kikao hicho ni kuwashirikisha wadau kuhusu tozo zinazohusiana na shughuli za Burudani na Sherehe, kwa lengo la kustawisha maendeleo ya Manispaa ya Shinyanga.
“Tumeitisha kikao hiki tukiwa na lengo la kuwashirikisha kuhusiana na mabadiliko ya tozo za sherehe na burudani, lengo letu kubwa ni kustawisha maendeleo ya Manispaa yetu,” amesema Luchagula.
Akinukuu kifungu cha Sheria, Luchagula amesema kuwa “Kwa mujibu wa Sheria ya fedha za Serikali za Mitaa (sura 290), Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ilitunga Sheria ndogo chini ya kifungu cha 6(1) na 16(1) cha Sheria hiyo iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 na kutangazwa katika gazeti la Serikali Na. 982 la Tarehe 13/12/2019 kuhusiana na tozo za shughuli na burudani.
“Hivyo, kwa mujibu wa kifungu cha Sheria hiyo (tajwa hapo juu), kuna shughuli ambazo bado hatujaingiza kwenye tozo hizo”, aliongeza.
Mbali na Luchagula, kikao hicho kilihusisha pia Washereheshaji (MC’s), Wapiga Muziki, Wamiliki wa Kumbi, Wamiliki wa Vifaa vya Muziki, Wapambaji pia Watendaji wa Kata.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga