- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na George Mganga, Shinyanga Manispaa
HALMASHAURI ya Manispaa ya Shinyanga imetunukiwa Cheti cha Ushindi wa Kwanza katika Mashindano ya Taifa ya Afya na Usafi wa Mazingira, katika kundi la Halmashauri za Manispaa Tanzania Bara, kwa kufikisha asilimia 87.
Tuzo hizo zilizoandaliwa na Wizara ya Afya, zilitolewa Jumamosi ya Novemba 19, 2022 jijini Dodoma kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe.
Cheti cha Ushindi kilichotolewa na Wizara ya Afya kwa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Katika ushindi huo, Manispaa ya Shinyanga ilizawadia kitita cha shilingi za kitanzania, milioni 15 (15,000,000) huku ikipatiwa na Kombe la Ushindi.
Baada ya kutangazwa kuwa mshindi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Dkt. Jomaary Mrisho Satura, amesema ushindi huo umetokana na jitihada kubwa ambazo watumishi wenzake wamekuwa wakizifanya huku akitoa pongezi kwao.
“Sina la kusema, kwa rehema hizi zisizohesabika za Mwenyezi Mungu. Mungu ametuwezesha kuwa wa kwanza kwa tuzo zote za mwaka huu kwa ngazi ya Manispaa.
“Matokeo haya ni kielelezo cha jitihada kubwa ya kazi kubwa na nzuri ambazo mmekuwa mkizifanya. Narejesha pongezi na shukrani nyingi kwenu.
"Nimekuwa nikiwaeleza, na hapa naomba kusisitiza kuwa hakuna aliyezaliwa kuwa wa mwisho katika maisha, Mungu anabariki jitihada na maandiko yanasema hivyo. Nawapenda na kuwathamini sana, ninyi ni kila kitu kwenye utendaji wangu,” amesema Satura.
Kombe la Ushindi lilikokabidhiwa na Wizara ya Afya kwa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mbali na kuwa mshindi wa kwanza wa Afya na Usafi wa Mazingira, Manispaa ya Shinyanga pia ilitangazwa kuwa mshindi wa kwanza wa Ukusaji wa Mapato kwa ngazi za Halmashauri katika mwaka wa Fedha uliopita.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga