- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na George Mganga, Shinyanga MC
KUELEKEA Maadhimisho miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Disemba 8, 2022 imeanza maadhimisho hayo kwa kupanda miti, kufanya usafi wa mazingira na kushiriki michezo mbalimbali.
Manispaa imepanda miti hiyo katika Kituo cha Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto ambapo Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Nchambi, ndiye alikuwa mgeni rasmi.
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Nchambi, akipanda mti kwenye eneo la kambi ya wazee Kolandoto.
Katika tukio hilo, Kativu Tawala Nchambi, amesema wameamua kupanda miti kwenye kambi ya wazee hao sababu walihusika katika kupigania Uhuru wa nchi, halikadhalika wanaijua vizuri historia ya taifa.
“Tumechagua kambi ya wazee Kolandoto sababu walihusika katika harakati za kupigania Uhuru wa Taifa na wanaijua vizuri historia yetu. Kijana aliyezaliwa leo hawezi ijua vizuri historia zaidi ya kusoma kwenye vitabu.
“Mpaka sasa nchi yetu imefanya maendeleo makubwa ya kuwatoa wazee kwenye magofu na kuwaweka kwenye nyumba bora, na katika mafanikio yote haya tangu uhuru, sisi kizazi chetu tumefyweka miti, tumeamua kuwapandia miti wazee wetu, nafikiri itakua na mvua itarejea. “Kesho ndiyo kilele cha miaka 61 ya Uhuru, kutakuwa na Kongamano kubwa la kujadili mafanikio ambayo nchi yetu imeyapata ndani ya miaka 61, wananchi wote mnakaribishwa”, amesema Nchambi.
Mbali na zoezi la kupanda miti, Ndg. Nchambi Pamoja na Kamati ya Usalama pia baadhi ya Maafisa kutoka Ofisi za Manispaa ya Shinyanga walihudhuria michezo mbalimbali katika Uwanja wa SHYCOM, Shinyanga, ikiwemo kukimbia na magunia, kukusanya chupa, mpira wa pete na miguu uliozikutanisha Shule za Sekondari Ngokolo na Uhuru, huku pia akiwepo Naibu Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Utaribu). Bw. Kaspar Kaspar Mmuya.Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru Tanzania Bara yatafanyika rasmi kesho katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM) kuanzia saa 2:00 asubuhi.
Naibu Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Utaribu). Bw. Kaspar Kaspar Mmuya, akizungumza na wanafunzi katika Uwanja wa SHYCOM.
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Nchambi, akitambulishwa kwa wachezaji wa Shule ya Sekondari Ngokolo kabla ya mchezo.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga