- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga inayo jumuisha mikoa miwili mkoa wa Shinyanga na Simiyu leo imezindua rasmi kuanza Kusikiliza Mashauri mbalimbali yanayohusiana na Sheria kwa Mwaka 2025.
Haya yamebainishwa Februari 03,2025 na Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu Kanda ya Shinyanga Jaji Frank Mahimbali wakati akizungumza kwenye kilele Cha wiki ya Sheria kwa Mwaka 2025 iliyofanyika Katika viwanja vya Mahakama kuu ya Tanzania Kanda hii ya Shinyanga, ambapo amewataka Majaji, Mahakimu na Mawakili kufanya kazi chini ya misingi ya viapo vyao.
“Maamuzi yetu lazima yatoe suluhisho, siyo kuchochea migogoro zaidi. Tunatakiwa tutatue migogoro badala ya kuwa chanzo cha migogoro, tunataka wananchi warudishe Imani kwetu kwa kuhakikisha tunawapa huduma bora kwa wakati. Maamuzi yetu yatoe suluhisho la migogoro na matatizo yaliyofikishwa mahakamani”,amesema Jaji Mahimbali.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro amesema Serikali ya mkoa wa Shinyanga inaridhishwa na mahakama kama mhimili wa dola wenye kufanya kazi katika kujenga ustawi wa mkoa.
Maadhimisho ya wiki ya sheria kwa mwaka 2025 yalikuwa yakiongozwa na Kauli mbiu .”Tanzania 2050: Nafasi ya Taasisi Zinazosimamia Haki Madai Katika Kufikia Malengo Makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo.”
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga