- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mafunzo ya namna bora ya ufugaji wa ng’ombe yametolewa jana tarehe 01-09-2023 na wataalamu wa mifugo kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, kwa hisani ya Mama O Dairies ambaye ndiye mfadhili mkuu wa Mafunzo hayo.
Akiongea katika Mafunzo hayo, Mjasiriamali na mmiliki wa kiwanda cha uzalishaji wa Maziwa cha Mama O Dairies Kilichopo Manispaa ya Shinyanga, aliwataka wafugaji kufanya ufugaji wenye tija kwa ajili ya ukuzaji wa kipato binafsi na Taifa kwa ujumla kwa kuzingatia usafi na afya ya wateja wao.
Kutokana na uzoefu wa ufugaji kwa muda mrefu ambao umemletea mafanikio, ameona ni vema ashirikishe wafugaji wenzake wa Manispaa ya Shinyanga kwa kualika wataalamu ili wawezeshwe kupata kile kilicho bora kwa manufaa yao.
Aidha wataalamu waliwasilisha mada mbalimbali kama vile namna ya utengenezaji wa chakula cha mifugo, namna bora ya ukamuaji wa maziwa, namna bora ya kukinga mifugo na magonjwa yanayoweza kusababisha vifo, namna ya kufanya mifugo ibaki kuwa na afya na kutoa maziwa kwa wingi pamoja na uhamilishaji.
Mada hizo ziliwasilishwa na wawezeshaji, ambao ni Chrispacy Kasimbazi – Afisa Mifugo wa Manispaa, Martin L. Elias – Daktari wa Mifugo Pamoja na Alex A. Kahama – Daktari wa Mifugo
Katika kikao hicho wafugaji walipata wasaha wa kutoa Mawazo, ushauri na maombi kwa uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga hasa katika kutengewa maeneo kwa ajili ya malisho ya mifugo yao.
Mwisho kabisa Mama O aliahidi kutoa ofa ya kufanya UHAMILISHAJI kwa wafugaji 150 bure. Uhamilishaji ni kitendo cha uzalishaji wa wanyama kwa njia ya kisasa kwa kutumia mbegu za madume bora ili kupata kizazi cha wanyama bora.
Hiyo ni fursa adimu sana. Kama wewe ni mfugaji jitahidi uwe wa kwanza kupata huduma hii kwa sababu ni huduma yenye gharama kubwa lakini imekuja kwako bure kabisa.
MATUKIO KATIKA PICHA
Mwezeshaji akitoa elimu kwa wafugaji
Washiriki wakisikiliza kwa Makini
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga