- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi wa Manispaa Ndugu Geoffrey Ramadhan Mwangulumbi amefungua mafunzo ya uboreshaji wa ukusanyaji wa mapato katika vyanzo vyote vilivyopo katika Manispaa ya Shinyanga. Mafunzo haya yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Lewis Kalinjuna ambapo wakuu wa Idara na vitengo na watumishi wanaohusika na ukusanyaji wa mapato wamehudhuria. Wakati wa kufungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Manispaa aliwataka watumishi waliohudhuria mafunzo kuitumia fursa hii ya mafunzo kujifunza kwa weredi na kisha baada ya mafunzo watumie ujuzi na elimu waliyoipata katika kuongeza mapato ya Halmashauri kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi wa Manispaa. "Wananchi wanahitaji huduma zetu, wananchi wanahitaji kuboreshewa mazingira yao ya kufanya kazi, wananchi wanahitaji huduma za Afya na elimu zilizo nzuri. Bila kuwa na fedha Halmashauri haitaweza kutoa huduma hizo. Kwa hiyo ni lazima tukusanye mapato ili tupate fedha za kuwahudumia wananchi". Alisema Mkurugenzi wa Manispaa.
Katika picha Mkurugenzi wa Manispaa akitoa neno la ufunguzi wa Mafunzo
Mafunzo haya yamefadhiriwa na mradi wa Benki ya Dunia kupitia kasma ya kujenga uwezo ambapo wataalam washauri wametoka katika timu ya Kanda inayoshughulikia mpango wa Uboreshaji wa miundombinu ya miji. Mradi huu unasimamia jumla ya Halmashauri 18 nchini ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ni mojawapo ya Halmashauri hizo zinazofadhiliwa. Baadhi ya miundombinu ambayo mradi huu unafadhiri ni ujenzi wa barabara za lami zilizojengwa katika kata ya Mjini.
Katika picha hapo juu Dr F.R Mubiru akieleza mada zitakazofundishwa wakati wa Mafunzo
Katika picha hapo juu ni baadhi wa washiriki wa mafunzo wakisikiliza mada kutoka kwa wataalamu washauri.
Ms. D. Kileo akifundisha namna ya uboreshaji wa ukusanyaji wa mapato
Baadhi ya washiriki wakisikiliza mada za uboreshaji wa ukusanyaji wa mapato
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga