- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mafunzo ya Uadilifu ya Viongozi wa Umma yametolewa kwa Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Divisheni na Vitengo katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambapo yanatajwa kuwa ni nguzo kuu katika utumishi na utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
Akitoa mafunzo hayo Katibu Msaidizi, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Ndg. Gerald Mwaitebele, amesema kuwa uzingatiaji wa maadili katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku kwa Waheshimiwa Madiwani na Watumishi wa Manispaa ya Shinyanga ukizingatia kuwa Manispaa inatekeleza miradi mikubwa kwa mapato ya ndani na kutoka Serikali kuu.
"Maadili ni dira, muongozo na kinga kwa Viongozi na watumishi iwapo wataamua kuyaishi na kwamba sasa wataweza kutimiza wajibu wao kikamilifu katika utekelezaji wa majukumu yao kwa Manispaa ya Shinyanga na Taifa kwa ujumla na hivyo kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Afisa Maadili katika Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Ndg. Vupala Mbwilo pamoja na mambo mengine aliwakumbusha baadhi ya faida za kuwa na Maadili ni pamoja na kutoa maamuzi sahihi bila upendeleo, uwajibikaji na uwazi, kufanya kazi kwa ushirikiano, kuheshimiana, kupendana katika utekelezaji wa majukumu yao.
Mbwilo alisema kuwa vitendo vingine visivyo vya Maadili ni pamoja na kupingana viongozi kwa kauli hadharani, kutopokea zawadi ya fedha taslimu isiyozidi Shilingi Laki Mbili, kuwa chanzo cha migogoro badala ya kuwa sehemu ya suluhisho.
Pia aliendelea kutaja vitendo visivyo na maadili kwa viongozi na watumishi kwa umma kuwa ni matumizi mabaya ya madaraka, kujipayia mali isivyo halali, kuweka shinikizo kwa mtumishi wa umma ili aadhibiwe au afukuzwe kazi kinyume na Sheria sambamba na kutumia lugha isiyofaa kama vile matusi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga