- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
WAKUU wa Divisheni na Vitengo katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, leo Februari 14, 2023 wamepatiwa mafunzo ya mfumo mpya wa TAUSI ambao umekuja na lengo la kufanya maboresho ya mfumo wa Ukusanyaji wa Mapato kwa Serikali za Mitaa (LGRCIS) unaotumika hadi sasa.
Mafunzo hayo yamewezeshwa na Wawezeshaji kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika katika Ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo kwenye Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Wawezeshaji wameeleza kuwa mfumo wa TAUSI umeaanzishwa ili kuondoa changamaoto zilizokuwa zinajitokeza kwenye mfumo wa LGRCIS, ikiwemo kuondoa orodha ya wadaiwa kwenye mfumo.
Aidha wameeleza kuwa mfumo wa TAUSI utamuwezesha mtuamiaji kuutumia popote, ambapo ukitumika vizuri utasaidia kuongeza mapato ya halmashuari.
Mafunzo ya mfumo huu mpya, yalianza rasmi Julai 13, 2022 na yanaendelea kutolewa mpaka sasa.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga