- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda S. Mwebea amewataka madiwani kuwasaidia wananchi, na kuwaelekeza namna ya kuomba mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na serikali kwa lengo la kuwakwamua kiuchumi.
Mhe. Mwebea ameyazungumza haya leo Oktoba 31, 2024 wakati akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwenye Kikao cha kwanza cha robo ( Julai Hadi septemba) 2024/2025 lililoketi Kupokea taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kila kata pamoja na kuwasilisha Changamoto zinazo wakabili wakazi wa kata hizo. ambapo amesema vikundi vingi vinakosa mikopo hiyo kwa sababu ya kutojaza vizuri taarifa kwa usahihi.
“Ninaushahidi wa kutosha hata kwenye kata yangu, vikundi vingi vinakosa sifa ya kupewa mikopo kwa sababu taarifa wanazojaza wanakosea au zinakuwa si sahihi, wengine wanajaza taarifa zao hazifanani, niwaombe sana waheshimiwa madiwani tuwasaidie wananchi kuwaelekeza namna ya kujaza fomu hizo, na namna ya kuomba Mikopo hiyo, lengo la serikali ni kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi ili kuondokana na umasikini”. amesema Mhe. Mwebea.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius R. Kagunze amesema serikali inajitahidi kupambana na upungufu wa watumishi ambapo jumla ya watendaji wa mitaa na vijiji 15 wameajiriwa.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga