- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MADIWANI SHINYANGA MC WAPITISHA MAPENDEKEZO MPANGO WA BAJETI MWAKA WA FEDHA 2024/2025 SH.BILIONI 40.3
Na. Shinyanga Mc
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo tarehe 25 Januari, 2024 limepitisha mapendekezo ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha (2024/2025) kiasi cha fedha Sh.bilioni 40.3 katika ukumbi wa mikutano wa Lewis Kalinjuna uliopo katika ofisi za Manispaa ya shinyanga.
Akiwasilisha mapendekezo ya mpango wa bajeti kwa mwaka 2024/2025 Kaimu Mchumi wa Manispaa ya Shinyanga Ndg. Michael Makotwe amesema wanatarajia kukusanya na kutumia kiasi cha fedha Sh.bilioni 40.3 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato.
“Tunatarajia kukusanya na kutumia kiasi cha fedha bilioni 40.3 kutoka vyanzo vya mapato vikiwemo mapato ya ndani Makisio ni kukusanya Sh.bilioni 6, Ruzuku na matumizi mengine Sh.bilioni 1.3, Ruzuku ya Mishahara Sh.bilioni 23.3, Ruzuku ya Miradi ya Maendeleo kutoka Serikali Kuu Sh. Bilioni 5.3 na Ruzuku ya Miradi ya Maendeleo Wahisani Sh.bilioni 4.3” amesema Ndg. Makotwe
Aidha, Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko mara baada ya madiwani kujadili mapendekezo ya bajeti hiyo na kuiridhia, alitamka rasmi kwamba Baraza hilo la Madiwani limeipitisha Bajeti hiyo huku akiwataka Madiwani pamoja na watendaji waisimamie vyema bajeti hiyo, pamoja na kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato na kubuni vyanzo vipya, ili mipango ambayo imepangwa iweze kutekelezeka na kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Kwa upande wake Katibu Tawala sehemu ya Ufuatiliaji wa Menejimenti na ukaguzi Mkoa wa Shinyanga Ndg. Ibrahimu Makana amewataka Madiwani pamoja na Watendaji kwamba wasimamie,kudhibiti na kufanya ukaguzi wa mapato, na wale wanaokusanya mapato fedha wawe wanaziwasilisha Benki kwa mujibu wa muongozo na kanuni.
Pamoja na mambo mengine Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhandisi Ndg. Kassimu Thadeo, amesema maoni yote ambayo yamejadiliwa kwenye kikao hicho cha Baraza la Madiwani watayazingatia na kuyafanyia kazi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga