- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Msitahiki Meya wa Halimashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko amewataka madiwani wote wa Halmashauri ya manispaa ya shinyanga kutokomeza utoro kwa wanafunzi kwa shule za Msingi na Sekondari.
Mhe. Masumbuko ameyasema hayo leo Julai 29,2024 katika kikao cha baraza la madiwani kwa robo ya nne ya mwaka 2023/2024 cha kuwasilisha taarifa za utendaji kazi katika kata zao, ambapo amesema katika Manispaa ya Shinyanga bado utoro kwa wanafunzi ni mkubwa na kuwataka madiwani kusaidiana na maafisa Elimu Msingi na Sekondari ili kupunguza na kutokomeza utoro.
“Watoto wengi hawaendi shule kwa sababu ya changamoto mbalimbali, sasa niwaombe waheshimiwa Madiwani twendeni tukasaidizane na maafisa elimu Msingi na Sekondari, tufanyeni jitihada za dhati kuhakikisha tunasaidiana kuondoa utoro kwa wanafunzi wetu kwani Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekwisha boresha mazingira mazuri katika sekta ya elimu”. Amesema Mhe. Masumbuko
Katika hatua nyingine madiwahi hao wamesema wanakabiliwa na changamoto za uhaba wa watendaji wa vijiji na mitaa ambapo wameiomba serikali kuwasaidia ili kupata watumishi hao.
Akitoa ufafanuzi wa upungufu wa watumishi Mkuu wa Division ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Ndg. Pius Sayayi amesema Halmashauri ya manispaa ya shinyanga kwa mwaka wa fedha 2024/2025 imepata kibali cha kuajiri watumishi 151 katika nafasi mbalimbali ikiwemo Watendaji wa Vijiji na Mitaa.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga