- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Maafisa waandikishaji wasaidizi Ngazi ya Kata Jimbo la Shinyanga Mjini wameahidi kufanya kazi chini ya taratibu na kanuni ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi pindi zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura litakapoanza kwa Jimbo la Shinyanga Mjini mnamo tarehe Agosti 21-27, 2024.
Wameyasema haya leo Agosti 15,2024 wakati wakiendelea na mafunzo ya vitendo kwa vifaa ambavyo vitakwenda kutumika katika Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura.
“Mafunzi haya ya siku mbili tumepata ujuzi juu ya kuingiza taarifa katika mfumo ili mwananchi aweze kupata kitambulisho na kupata haki yake ya msingi ya kupiga kura,kwa niaba ya maafisa wenzangu ngazi ya kata tutakwenda kufanya kazi chini ya utaratibu na kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.” Amesema Christina Kessy, Afisa Mwandikishaji Msaidizi kata ya Kambarage
Akifunga mafunzo haya Afisa Mwandikishaji Jimbo la Shinyanga Mjini Mwl. Alexius Kagunze amewataka Maafisa waandikishaji hao kutumia muda wao wa ziada kujikumbushia mambo walioelekezwa katika mafunzo haya ili kuongeza uelewa zaidi juu ya zoezi zima la Uandikishaji na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
“Maafisa Wasaidizi wote ngazi ya Kata tumieni muda wenu wa ziada kujikumbushia na kupitia maelekezo yote mliyopewa ,hiyo ndiyo zana kuu ya kufanya kazi yenu kwa ufasaha”. Amesema Mwl. Kagunze
Mafunzo haya yamefanyika kwa siku mbili tarehe 14-15 Agosti 2024 katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga mafunzo ambayo yamewakutanisha Maafisa Tehama,Maafisa Ugavi wataalamu kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), ambao walikuwa wakitoa mafunzo kwa Maafisa waandikishaji ngazi ya kata Jimbo la shinyanga Mjini.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga