- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
LAAC YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA SHINYANGA.
Na. Jesca Kipingu SHYMC
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Pongezi hizo zimetolewa na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya LAAC, Mhe. Staslaus Mabula (MB) leo tarehe 27 Marchi, 2024 wakati akikagua ujenzi wa Soko kuu la Shinyanga na shule ya sekondari ya wasichana Shinyanga pamoja na Miundombinu mbalimbali inayoendelea kukamilishwa katika shule hii.
“Niwapongeze kwa usimamizi mzuri wa miradi hii hakika shule inamajengo mazuri na yenye kuendana na thamani ya fedha iliyotolewa na serikali , mafundi wazuri wenye utendaji kazi mzuri pamoja na ujenzi mzuri wa mabanda ya soko ambao mnatumia kujenga kwa kupitia mapato ya ndani na kusaidi ujenzi huu kuleta tija nzuri kwa wananchi kwa ujumla.” amesema Mhe. Mabula
Pamoja na mambo mengine kamati ya LAAC imeshauri Halmashauri zengine zije kujifunza namna bora ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye kuleta tija na inayozingatia thamani ya fedha zinazotolewa na serikali.
Aidha, Kamati imetoa maelekezo kwa ajili ya kuboresha sehemu mbalimbali katika miradi hii, huku ikitaka majengo yote yaendelee kutunzwa vizuri na kwa uzalendo kwa ajili ya vizazi vijavyo na kuhakikisha wanafunzi wote katika shule ya wasichana Shinyanga wanamaliza wote na kwa ufaulu mzuri ili kuendeleza jitiada nzuri za Kumuunga mkono Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwekeza vizuri sekta ya elimu.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elius Masumbuko kwa niaba ya baraza la madiwani, Menejiment na Watumishi wa Manispaa ameishukuru kamati kwa ukaguzi mzuri wa miradi na kuhaidi kwenda kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Kamati.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga