- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
KU YA WILAYA NA KAMATI YA MAAFA YA MANISPAA YA SHINYANGA YAWATEMBELEA WALIOKUBWA NA MAAFA.
Na. Shinyanga Mc
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Shinyanga ikiongozwa na katibu Tawala wa wilaya Ndg. Saidi Kitinga kwa niaba ya Mkuu wa wilaya akiambatana na Kamati ya Maafa ya Manispaa ya Shinyanga leo tarehe 18 Oktoba, 2023 imetembelea kaya zilizokubwa na maafa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha jana.
Akiongea katika ziara hiyo Ndg. Revocatus Lutunda Mratibu wa Kamati ya Maafa ambae ni MKuu Divisheni ya kilimo na Uvuvi Manispaa ameeleza kwamba mvua iliyonyesha jana imeleta madhara kwa baadhi ya kaya na kuwaomba wananachi waendelea kuchukua tahadhari ya kutoka kwenye makazi ambayo yapo mabondeni pamoja na kutoka kwenye nyumba ambazo ni hatarishi katika kipindi hiki cha mvua.
" Niwaombe wananchi wote kwa ujumla endeleeni kuchukua taadhari ya mvua zinazoendelea kunyesha kwa kutoka kwenye makazi yaliopo mabondeni pamoja na makazi ambayo sio rafiki katika kipindi hiki cha mvua"
Aidha, Ndg. Lutunda amesisitiza kwa kuwataka watendaji wa kata, vijiji na Mitaa kuendelea kubaini maeneo yote hatarishi lakini pia kamati za maafa za kata kufanya kazi bila kuchoka ili kuepukana na madhara yoyote ambayo yatazidi kutokea pamoja na kuwaomba wananchi kulima mazoa yanaweza kuimili mvua nyingi zinazoendelea kunyesha.
Kwa upande wake Katika Tawala wa Wilaya Ndg. Kitinga amewaomba wanachi katika kipindi hichi cha mvua wachemshe maji ya kunywa ili kuepuka magonjwa ya mlipuko kwani mvua zinaponyesha zinachafua vyazo vya maji na miundombinu ya maji, kuboresha vyoo , kuhifadhi vyakula pamoja na kuwashauri wajenge nyumba zenye msingi imara.
Awali kamati hizi ziliweza kutembelea kata ya Mwawaza katika kijiji cha Mwawaza pamoja na Kata ya Mwamalili katika kijiji cha Mwamalili ambapo baadhi ya nyumba ziliezuliwa na mvua na kusababisha madhara kwa baadhi ya kaya kuumia ambapo walipelekwa hospital kwa ajili ya matibabu na wanaendelea vizuri.
Angalizo kwa Wananchi wote kwa ujumla kwa kutoka katika maeneo ya mabondeni pamoja na kutengeneza vizuri mifereji inayopitisha maji kwa usahihi ili kuepuka na mafuriko katika makazi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga