- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
KITENGO CHA TEHAMA WAKISHIRIKIANA NA BAADHI YA WATUMISHI WA MANISPAA YA SHINYANGA WATOA BIMA ZA AFYA KWA KAYA ZENYE UHITAJI
Na.Shinyanga Mc
kitengo cha Tehama na baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Shinyanga leo tarehe 18 Agosti, 2023 wametoa bima za afya iCHF iliyoboreshwa kwa kaya zenye uhitaji katika zahanati ya Chamaguha iliyopo kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga.
Akiongea katika kukabidhi bima hizo Afisa Tehama Ndg. Boniphace Marago kutoka Manispaa ya Shinyanga ameeleza kwamba afya ni mtaji na msingi wa maisha kwa binadamu afya ikiwa nzuri basi kila kitu kitafanyika kwa juhudi kubwa lakini afya ikiwa mbaya basi kila kitu nacho hakitaweza kufanyika kwa ustadi mzuri.
"Afya ni msingi na mtaji mkubwa kwa binadamu ili binadamu aweze kufanya majukumu yake ya kila siku anahitaji kuwa na afya nzuri" alisema Marago
Kwa Upande wake Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Chamaguha Dk. Frida Olomy ameishukuru sana kitengo cha Tehama na watumishi baadhi wa Manispaa waliojumuika katika kutoa bima za afya kwa kaya zenye uhitaji kwa kuichagua Chamaguha kwani wangeweza kwenda kata nyengine lakini wameona waje kutoa msaada kata ya chamaguha hakika amefarijika sana na kuwaomba wanufaika hao wa bima wazitunzi vizuri.
Ikumbukwe Bima ya afya iCHF hutolewa kwa Zahanati, Vituo vya afya na Hospitali za Serikali tu, awali Bima hii ilianzishwa katika Mikoa mitatu kama majaribio ikiwemo Mikoa ya Dodoma, Morogoro na Shinyanga baada ya kuona muitikio ni mkubwa ndipo Mikoa mingine ilifuata kutoa bima pia bima hii hupatikana kwa kiasi cha Tsh 30,000 kwa kila kaya ambayo inajumuisha watu sita na hutumika kwa mwaka mmoja.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga