- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kamati ya ushauri ya wilaya ya Shinyanga (DCC) ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro imeadhimia na kuzitaka taasisi za Serikali ikiwemo Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA, Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) Pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wilaya ya Shinyanga kuwasilisha mpango mkakati juu ya upatikanaji wa huduma kwa maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma kabla ya machi 30,2025.
Maagizo haya yametolewa leo Februari 25,2025 Katika kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya ya Shinyanga kilichoketi kwa lengo la Kupokea mapendekezo ya bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/2026 kikao kilichofanyika Ukumbi wa mikutano wa Lewis Kalinjuna uliopo ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya shinyanga.
Katika hatua nyingine kamati hiyo imeitaka Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Shinyanga SHUWASA kuona umuhimubwa kukamilisha mradi wa kuchakata kinyesi unaotekelezwa kata ya Kizumbi ndani ya Manispaa ya Shinyanga ili uweze kukamilika na kutoa huduma.
Sambamba na hayo kamati hiyo imeshauri agenda ya lishe kwa wanafunzi iwe ya kudumu katika vikao mbalimbali lakini pia iingizwe Kwenye fomu za kujiunga na shule kwa lengo la Kuimarisha afya za wanafunzi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga