- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA NA MASWALA YA UKIMWI YATEMBELEA MANISPAA YA SHINYANGA
Na. Shinyanga Mc
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Maswala ya Ukimwi leo tarehe 11 Oktoba, 2023 imefanya ziara ya kutembelea na kukagua vikundi vya mabinti waliokuwa wanaishi kwenye mazingira hatarishi ya uwezekano wa kupata maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.
Akizungumza katika ziara hiyo Mhe. Stanslaus Nyongo Mwenyekiti wa Kamati na pia ni Mbuge wa Maswa Mashariki ameeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan anafanya jitihada kubwa katika kumlinda mtoto wa kike asipate changamoto hatarishi , hivyo wanahakikisha watoto wakike wanaoishi katika mazingira hatarishi wanapata elimu ya mabadiliko ya tabia na kutoka katika mazingira hatarishi kupitia wadau mbalimbali .
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anafanya jitihada mbalimbali katika kumlinda mtoto wa kike kwa kutoka kwenye mazingira hatarishi”alisema Mhe. Nyongo
Aidha, Mhe. Nyongo amewataka wanakikundi hao kuwa mabalozi wa mabinti wengine wanaoishi katika mazingira hatarishi kwa kuwapitia elimu walizopata ikiwemo elimu ya akiba ya uchumi, elimu ya mabadiliko ya kitabia, ujasiliamali pamoja na kuwataka wasirudi nyuma na kuwa na tabia mbaya bali wazingatie yote waliofundishwa na kuendelea kupinga mila na desturi zinazoleta hali hatarishi.
Kamati hiyo iliweza kukagua na kutembelea vikundi vitatu vikiwemo kikundi cha Sitetereki kilichopo Old Shinyanga kinachofanya ujasiliamali wa vitu mbalimbali ikiwemo kushona mapochi,sabuni za maji, kikundi cha Jahaza ibadakuli ambacho kinatengeneza sabuni za vipande, viatu na ushonaji wa nguo, pamoja na kikundi cha Tunaweza kolandoto kinachotengeneza majiko ya udogo na vyungu.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga