- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
KAMATI YA FEDHA NA UTAWALA YA MANISPAA YA SHINYANGA YAFURAHISHWA NA UTEKELEZAJI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO.
Na. Shinyanga Mc
Kamati ya Fedha na Utawala ya Manispaa ya Shinyanga ikiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa Mhe. Elias Masumbuko yafurahishwa na utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika manispaa.
Akizungumza katika ziara hii Mhe. Masumbuko ameeleza kwamba wamefurahishwa na utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo na kuwaomba wasimamizi wa miradi hiyo kuendelea kusimamia kwa ukaribu ili kuepukana na changamoto yoyote itakayoweza kujitokeza, huku akiwata mafundi kuongeza kasi ya ujenzi kwa sababu kila kitu kipo.
"Tumefurahishwa na utekelezaji mzuri wa miradi yote tuliyoitembelea na kuikagua hakika mnastahili pongezi niwaombe wasimamizi wote wa miradi muendelee kusimamia kwa ukaribu zaidi ili kuepukana na changamoto mbalimbali na niwatake mafundi kuzidi kuongeza kasi ya ujenzi ili miradi ikamilike kwa wakati ianze kutumika" alisema Mhe. Masumbuko
Aidha, kamati hii iliweza kutembelea miradi ya maendeleo Sekta ya afya ikiwemo ujenzi wa jengo la dharula EMD katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga pamoja na Sekta ya Elimu kwa kutembelea na kukagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari ngokolo B inayojengwa katika kata ya Ndembezi mtaa wa Butengwa pamoja na kukagua ujenzi wa miundombinu mbalimbali unaoendelea kujengwa shule ya Sekondari ya wasichana Shinyanga.
Lengo la ziara hii ni kuangalia hatua ipi imefikia ya utekelezaji wa miradi, kutoa ushauri mbalimbali pamoja na kutilia nguvu palipokuwa na changamoto
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga