- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
KAMATI YA FEDHA NA UTAWALA YA MANISPAA YA SHINYANGA YAFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO.
Na. Shinyanga Mc
Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ikiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa Mhe. Elias Masumbuko leo tarehe 7 Februari, 2024 wametembelea na kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga, Soko la wajasiriamali Ibinzamata, ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika shule ya wasichana shinyanga pamoja na kutembelea shule mpya ya sekondari Butengwa.
Pamoja na mambo mengine mwenyekiti wa kamati ya fedha na Utawala Mhe. Elias Masumbuko kwa niaba ya Baraza zima la Madiwa wa Manispaa ameipongeza uongozi mzima wa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga kwa usimamizi mzuri wa fedha kwani kiasi kilichopangwa kutumika katika ujenzi wa jengo la dharula (EMD) ambapo jengo hilo limekamilika, zimeweza kubaki na kuanza ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD).
Lengo la ziara hii ni kuangalia hatua ipi imefikia ya utekelezaji wa Miradi pamoja na kutilia nguvu pale palipokuwa na changamoto na kutoa ushauri wa mambo mbalimbali.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga