- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kamati ya Fedha na Utawala Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imeazimia kuboresha bwawa la Ibadakuli kwa madhumuni ya kutumika kama kama chanzo kipya cha mapato kwa Halmashauri, kituo cha utalii wa ndani, pamoja na kuimarisha matumizi yake kama chanzo endelevu cha maji kwa wananchi.
Uamuzi huu umetolewa na wajumbe wa kamati hiyo wakati wa ziara ya kamati iliyofanyika kwa lengo la kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo tofauti ndani ya Manispaa.
Akizungumza katika ziara hii, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Masumbuko, ameeleza kuwa Halmashauri imelenga kuweka mazingira rafiki ya matumizi ya bwawa hilo kwa ajili ya shughuli za kiuchumi ikiwemo ufugaji wa samaki, utalii wa ndani, pamoja na kutoa huduma za burudani kwa jamii.
“Ni muhimu sana wataalamu wetu kuharakisha mipango ya uboreshaji wa bwawa hili. Bwawa la Ibadakuli lina maji ya kutosha msimu wote wa kiangazi na masika. Tukiliendeleza vizuri, linaweza kuwa chanzo kikuu cha mapato na sehemu ya kuwavutia watalii katika Manispaa yetu kulingana na ubunifu wetu,” amesema Mhe. Masumbuko.
Katika hatua nyingine, kamati hiyo imetembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya sekta ya elimu, ukiwemo, Ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika Kata ya Kizumbi, unaogharimu kiasi cha shilingi milioni 103,890,563 fedha kutoka Serikali Kuu; Ujenzi wa mabweni manne katika pamoja na matundu 12 ya vyoo Shule ya Sekondari Rajani, kwa ajili ya kuongeza nafasi kwa wanafunzi wa bweni; ambapo kukamilika kwa mabweni hayo yatahudumia jumla ya wanafunzi 480.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Ndg. Peres Kamugisha,ameahidi kuongeza usimamizi wa karibu kwa wakandarasi wote ili kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa viwango vya ubora vinavyotakiwa na kwa muda uliopangwa.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga