- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ikiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ambaye ndio mwenyekiti wa kamati Mhe. Elias Masumbuko leo tarehe 18 Julai, 2024 wametembelea na kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya shinyanga.
Mhe. Masumbuko ameipongeza menejimenti ya manispaa kwa ujumla kwa usimamizi mzuri wa miradi yote waliyoitembelea pamoja na kuitaka menejimenti kuweka mabango ya ujenzi kwa lugha ya kiswahili ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kukuza lugha ya kiswahili, huku akiwataka mafundi kuongeza kasi ya ujenzi ili majengo hayo yaanze kutumika pamoja na kujenga majengo mazuri yenye ubora kwa kuzingatia thamani ya fedha iliyotolewa na serikali.
Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga, ujenzi wa Zahanati ya Mwamagunguli katika kata ya Kolandoto pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika shule ya wasichana shinyanga.
Lengo la ziara hii ni kuangalia hatua ipi imefikia ya utekelezaji wa Miradi pamoja na kutilia nguvu pale palipokuwa na changamoto na kutoa ushauri wa mambo mbalimbali.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga