- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imetembelea Mradi wa Machinjio ya Kisasa Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga na kuuagiza Uongozi wa Manispaa hiyo kufanya jitihada za maksudi kuimarisha eneo la Masoko kwa kuongeza idadi ya ng’ombe na mbuzi wanaotakiwa kuchinjwa ili mradi ulete tija.
Akizungumza baada ya Wajumbe wa LAAC waliombatana pia na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Festo Dugange kutembelea Mradi huo leo Ijumaa Machi 18,2022, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mhe. Selemani Zedi amesema licha ya kukamilika kwa mradi huo lakini wamebaini kuwa idadi ya ng’ombe wanaotakiwa kuchinjwa haitoshi ukilinganisha na uwezo wa machinjio hiyo.
“Tumeona mradi umekamilika na umeanza kufanya kazi lakini tulichobaini ni kwamba mradi ni mkubwa, una uwezo mkubwa lakini kwa sasa hakuna ng’ombe na mbuzi wa kutosha kufikia kiwango cha uzalishaji kilichopo.
Kamati inafahamu kwamba hii miradi ya kimkakati ambayo fedha zilitoka Benki ya Dunia ambapo halmashauri nyingi ikiwemo hii ya Manispaa ya Shinyanga ilipata na kuanzisha miradi na nyinyi Shinyanga mlianzisha Mradi wa machinjio ya kisasa lengo lake lilikuwa Halmashauri itengeneze miradi ili hiyo miradi igeuke kuwa vyanzo vya mapato”,
“Sasa mradi wa Machinjio umekamilika, ushauri wetu ni kwamba zifanyike jitihada za maksudi, lazima mpate watu wa masoko wazuri wanaoweza kuisukuma vizuri, wapite huko na huko ili mpate ng’ombe na mbuzi wa kutosha wa kuchinja kwa sababu mradi huu una uwezo wa kuchinja ng’ombe 500 kwa siku lakini sasa mnachinja ng’ombe 20 kwa siku na pia wanatakiwa kuchinjwa mbuzi 1000 lak
ini sasa mnachinja mbuzi 38 kwa siku”,amesema Zedi.
Ameongeza kuwa lengo la miradi ya kimkakati ni kuzifanya halmashauri zijitegemee ziwe na vyanzo vya mapato hivyo kuutaka uongozi wa Manispaa ya Shinyanga kuongeza ubunifu ili mradi huo uwe na manufaa zaidi.
“Tunajua Menejimenti, Mkurugenzi wa Manispaa na timu yako, Mkuu wa wilaya na Mkuu wa Mkoa huu mradi mmeukuta kwa jinsi mlivyojieleza, kamati ina imani na utendaji kazi wenu, tunajua mna uwezo wa kuibadili hii hali ya machinjio hii ili ilete tija.Tunakupongeza Mkurugenzi kwa kushirikisha Waheshimiwa Madiwani na hata kwenye hii ziara wapo tunajua haya tuliyoyaacha waheshimiwa madiwani wataendelea nayo”,amesema Zedi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga