- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Jumuiko la watumishi wa Manispaa ya Shinyanga limefanyika Leo tarehe 07/08/2021 katika viwanja vya Mazingira Centre ambapo mambo kadhaa yameainishwa likiwemo suala la aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Kuwaaga Watumishi aliowaongoza kwa muda wa miaka mitano
Aidha Mkurugenzi aliyepita alikabidhiwa hati ya Pongezi kwa kuwa kiongozi mwenye maono na muibuaji wa miradi mbalimbali yenye tija katika Manispaa ya Shinyanga.
Idara mbalimbali zilimpongeza na kumpatia zawadi kemkem ikiwa ni ishara ya Upendo kwa Kiongozi wao ambae aligusa wengi kwa namna tofauti.
Mkurugenzi alionekana kuwa na furaha wakati wote alipokuwa akiwaaga Watumishi na Kuwaasa kuendelea kuchapa kazi,pia aliahidi kutoa ushirikiano wakati wote atakapohitajika kufanya hivyo.
Aidha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, mh. Nkulila alipata fursa ya kumpongeza Mkurugenzi aliepita kwani anaifahamu vema kazi yake njema kwa muda wote toka alipoingia Manispaa ya Shinyanga mwaka 2016.
Mkurugenzi mpya wa Manispaa ya Shinyanga Ndg. Jomaari Mrisho Satura Ameahidi kuendeleza Mazuri aliyoyaacha Mwenzake ili kufikia lengo la kuifanya Manispaa ya Shinyanga kuwa Jiji
Mgeni Rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Amewataka watumishi kushikamana na kufanya kazi kwa Pamoja na kwa ushirikiano.
Zawadi zilitolewa kwa Washindi walioshinda mashindano mbalimbali Kitaifa, Kimkoa na Kihalmashauri.
MATUKIO KATIKA PICHA
Kwaya ya Waalimu Ikitumbuiza siku ya Jumuiko
Viongozi wakiwa wamewasili tayari kwa Ufunguzi wa Jumuiko la Watumishi
Watumishi na Wageni mbalimbali wakiwa wamewasili katika viwanja vya Mazingira Center
Ndugu Geoffrey Mwangulumbi akitoa neno la Shukrani kwa Watumishi na Viongozi Wakati wa Jumuiko la Watumishi
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto kutoka shule ya Sekondari Uhuru Tanzania akihutubia siku ya Jumuiko la Watumishi
Mvumbuzi wa Mashine ya Kukunia Nazi inayotumia Umeme ambayo ilishinda Kitaifa katika
Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi na Teknolojia (MAKISAT) akielezea uvumbuzi wake
Mshindi wa Miruko ya Juu (Long Jump) Kitaifa katika Mashindano ya UMISETA Akielezea namna alivyoshinda
na mahitaji yatakayomwezesha kutimiza ndoto zake
Tuzo zikitolewa kwa Washindi katika Mashindano mbalimbali
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga