- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
“JIEPUSHENI NA MIKOPO KAUSHA DAMU “ RC MNDEME
Na. Shinyanga Mc
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewataka wanawake wa mkoa wa shinyanga kujiepusha na mikopo ya kausha damu kwani inachangia kurudisha nyuma katika kujikwamua kiumchumi.
Mhe. Mndeme amezungumza hayo leo tarehe 8 March, 2024 katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambapo kimkoa kwa Shinyanga yamefanyika katika Viwanja vya Sabasaba kambarage katika Manispaa ya Shinyanga na kuwataka Wanawake mkoani humo wawe wavumilivu katika kipindi hiki cha mpito, ambapo Serikali inaendelea kufanya maboresho juu ya utoaji wa mikopo ya asilimia 10 na wasijiingize kwenye mikopo kausha damu.
“Mnamo mwezi Aprili 2023 Serikali ilisitisha utoaji wa mikopo asilimia 10 ya Mapato ya ndani ya halmashauri kwa makundi ya Wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu, na ilisitisha kwa lengo Mahususi la kuboresha utoaji wa mikopo hii, na pia kufuatilia marejesho ya mikopo ili kuhakikisha mzunguko unakuwa endelevu,” amesema Mhe. Mndeme
Aidha, Mhe. Mndeme ametoa Maagizo kwa Wakuu wa Wilaya Mkoani humo, kwamba wasimamie uanzishaji wa Majukwa ya Wanawake Kiuchumi kuanzia ngazi ya Kata, sababu yanawaimarisha wanawake na kuwapa nguvu pamoja na kuinuka kiuchumi.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa, amempongeza Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwa amini Wanawake na kuwapatia fursa mbalimbali za uongozi, na wamewakuwa wakifanya vizuri kwa kuiga uongozi wake na kuwatumikia wananchi katika kuleta Maendeleo.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Shinyanga Ndg. Grace Bizulu, amewataka wanawake kuendelea kujitambua na kujiheshimu kwa kuendelea kuwalea watoto katika maadili mema huku akimshukuru Rais kwa kuwekeza katika elimu na kuwaomba wanawake kuendelea kuwahimiza watoto kupenda shule na kila mmoja kwa nafasi yake asimame katika kupiga ukatili wa kijinsia.
Kila ifikapo tarehe 8 March wanawake wote duniani husherekea siku ya wanawake duniani ambapo kwa mwaka huu 2024 Kauli mbiu inasema “Wekeza kwa Wanawake,Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii,”
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga