- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
ICS YATOA VYEREHANI KWA MABINTI WANAOTOKA MAZINGIRA MAGUMU MANISPAA YA SHINYANGA.
Na. Shinyanga Mc
Shirika linalotekeleza afua za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa kuwajengea uwezo wazazi, walezi, mabinti , watoto na jamii kwa ujumla (ICS) leo tarehe 15, Mei 2024 katika kusherekea siku ya familia duniani imetoa vyereheni 7 kwa wasichana wanaotoka katika mazingira magumu, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Lewis Kalinjuna katika ofisi za Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza katika hafla hii Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko ambae ndio mgeni rasmi wa hafla hii ameishukuru Taasisi ya ICS kwa kuweza kuendelea kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na watoto huku akiwasihi mabinti waliopatiwa vyerehani kwa ajili ya kujiendeleza na fani walioipata kwenda kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza ndoto zao.
“Kipekee niwapongeze taasisi ya ICS kwa kuendelea kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto na niwasihi mabinti wote mliopata bahati hii ya kuweza kupata ujuzi wa ushonaji nendeni mkafanye kazi kwa bidii na uaminifu ili muweze kutimiza ndoto zenu.” amesema Mhe. Masumbuko
Awali, Meneja wa shirika la ICS Bi. Sabrina Majikata ameeleza kwamba kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga waliweza kuwapata ma binti wanaotoka mazingira magumu na kuweza kuwadhamini kwa kuwapatia mafunzo ya fani ya ushonaji cherehani katika chuo cha veta pamoja na kuwapatia vifaa vya ushonaji na mahitaji mbalimbali yaliyohitaji katika fani ya ushonaji.
“ Tunaishukuru ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa kwa msaada wake kupitia maafisa maendeleo ya jamii kwa kuweza kuwapata mabinti hawa na sasa wameweza kupata mafunzo ya fani ya ushonaji na tumeweza kuwagharamia mahitaji yote muhimu yaliyokuwa yanahitajika katika matumizi ya ushanaji ambayo yameweza kugharimu kiasi cha Tsh. 6,400,000/= amesema Bi. Majikata
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga