- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji wa Kondoa na wakuu wa ldara na Vitengo wa Halmashauri hiyo wamefanya ziara Manispaa ya Shinyanga kujifunza namna ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kupitia mapato ya ndani ya Manispaa pamoja na usimamizi wa usafi wa mazingira.
Akizungumza leo Novemba 30,2024 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa Bi.Jovita B. Buyobe ameipongeza Manispaa ya Shinyanga kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo kupitia mapato ya ndani lakini pia namna ambavyo Manispaa inafanya jitihada ya kutunza mazingira kupitia usafi wa mazingira na upendezeshaji Mji kupitia fedha za ndani ya Halmashauri.
“Kiukwel nitakuwa mchonyo wa fadhila kama nisipo ipongeza Manispaa hii kwa utekelezaji wa miradi bora na ya Kisasa kupitia mapato ya ndani manispaa, wakati tunaingia shinyanga nilivutiwa na namna ambavyo maeneo yao yalivyo safi na yanavutia hakika viongozi mnastahili pongezi kubwa jitihada zenu zinastahili kushika nafasi ya kwanza katika tuzo za usafi na ndomaana leo tupa hapa kwa ajili ya kujifunza namna bora utekelezaji wa miradi na kubadilishana uzoefu wa mambo mbalimbali “. Amesema Bi. Buyobe.
Kwa upande wake Mstahiki Meya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko amesema kupitia ubunifu wa wataalamu wa halmashauri ufuatiliaji na matumizi sahihi ya fedha tumefanikiwa kupanda ukusanyaji mapato kutoka bilioni 2 kwa Mwaka 2019/2020 hadi Bilion 6 kwa Mwaka wa fedha 2023/2024, pamoja na matumizi ya vikundi vya usafi vilivyo chini ya usimamizi wa Manispaa ndiyo siri ya kushinda tuzo ya mshindi wa kwanza kwa usafi wa mazingira kati ya Halmashauri zote nchini kwa mwaka wa pili mfululizo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Ndg. Peres Kamugisha amewashukuru sana uongozi wa halmashauri ya Mji wa Kondoa kuichagua Manispaa ya kuwa sehemu ya kujifunza huku akitumia fursa hiyo kuziomba halmashauri zingine kutembelea Manispaa ya Shinyanga ili kujifunza zaidi kwa ustawi wa taifa kwa ujumla.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga