- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA INATARAJIA KULIPA RUZUKU KWA WALENGWA WA TASAF
Na. Shinyanga Mc
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga inatarajia kulipa ruzuku kwa walengwa katika mpango wa kunusuru kaya masikini (TASAF) muda wowote kuanzia tarehe 9/08/2023.
Haya yamesemwa leo na Afisa ufuatiliaji TASAF kwa upande wa Shinyanga Manispaa na Halmashauri ya wilaya ya shinyanga Bi Tabu Maro katika kikao cha waandishi wa Habari kilichofanyika leo tarehe 7 Agosti, 2023 katika ukumbi wa kalinjuna uliopo katika ofisi za Manispaa ya shinyanga.
"Tunatarijia kufanya malipo kwa walengwa wa tasaf zaidi ya 3900 muda wowote kuanzia tarehe 9/08/2023 hivyo tunaomba walengwa wote ambao wapo mbali na makazi yao ya kudumu warudi mapema kwani malipo kwa kipindi hiki tunahitaji kila mmoja awepo ili kuhakiki taarifa zao" alisema Bi Tabu
Kwa Upande wake Mratibu wa Tasaf Manispaa ya Shinyanga Bi Octavina Kiwone ameeleza kuwa malipo yanayoenda kulipwa ni ya awamu mbili ambapo amesema watalipwa ya mwezi wa 3 ,4 na mwezi wa 5 na 6 na kuwaomba walengwa wote wahakikishe wanasaini nyaraka za malipo na kupewa za awamu zote mbili ili kuepuka usumbufu wowote utakao jitokeza .
Pamoja na mambo mengi Bi Octavina ametoa tahadhari kwa walengwa kuhakikisha wanatoa taarifa zao zinazofanana na zile zinazosoma katika namba zao za nida na sio vinginevyo, pia amewataka watendaji wa kata, mitaa na wenyeviti wa serikali za mitaa kuanza kutoa taarifa mapema kwa walengwa ili malipo yatakapoanza walegwa wote wahudhurie bila kukosa na washiriki warsha za jamii kama taratibu zinavyoelekeza.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga