- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
"HAKIKISHENI KILA ANAYEINGIZWA KWENYE MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI TASAF AWE ANASIFA ZINAZOHITAJIKA" DC SAMIZI
Na. Shinyanga Mc
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi amewataka wakazi wa kijiji cha Bugayambelele Kata ya Kizumbi kuzingatia sifa na vigezo vinavyohitajika katika kuwaingiza walengwa katika mpango wa kunusuru Kaya masikini yani TASAF .
Mhe. Samizi ameyasema hayo leo tarehe 16 Oktoba, 2023 alipofanya ziara ya kukagua na kutembelea ujenzi wa zahanati ya Bugayambelele unaojengwa kupitia nguvu za wananchi pamoja na wadau mbalimbali ambapo alipata muda wa kusikiliza kero za wananchi wa kijiji hicho, moja ya kero ni baadhi ya walengwa wanaoingizwa kwenye TASAF hawana vigezo na badala yake kuwaacha watu wenye vigezo.
"Hakikisheni kila anayeingizwa kwenye mpango wa kunusuru Kaya masikini TASAF anakidhi sifa na vigezo vinavyohitajika na sio vinginevyo " alisema Mhe. Samizi
Pamoja na mambo mengine Mhe. Samizi alipata wasaa wa kutembelea kijiji cha mwamashele kata ya kizumbi kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi ambapo wananchi wa kijiji hicho waliwasilisha mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na kambi ya jeshi iliyopo katika kijiji hicho.
Aidha, Mhe. Samizi alipokea Malalamiko ya mgororo huo na kuwaahidi wananchi kuwa atakwenda kuufanyia kazi kwa kushirikina na kamati ya kijiji hicho iliyoundwa kwa dhumuni la kutatua mgogoro huo.
Ziara hii ya Mhe. Samizi ni mwendelezo wa ziara zake kwa lengo la kukagua, kutembelea miradi ya maendeleo na kufanya mikutano ya hadhara kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga