- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
FCC YATOA MAFUNZO KWA WADAU WA BIASHARA MANISPAA YA SHINYANGA
Na.Shinyanga Mc
Tume ya Ushindani (FCC) leo tarehe 30 Novemba, 2023 imetoa mafunzo kwa wadau wa biashara katika ukumbi wa Kalinjuna uliopo katika ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Akifungua Mafunzo haya Kaimu Mkurugenzi Bi. Getruda Gisema ameipongeza tume ya ushindani (FCC) kwa kuandaa mafunzo haya kwa wadau wa biashara ili kuwajengea uwezo wa kutambua bidhaa bandia na bidhaa halisi huku akiwasihi washiriki kusikiliza kwa makini ili wanaporudi katika biashara waweze kutambua mambo mbalimbali ikiwemo bidhaa bandia.
"Niwapongeze Tume ya Ushindani (FCC) kwa kuandaa mafunzo haya kwa wadau wa biashara ili kuweza kuwapatia uelewa wa kutambua bidhaa bandia hii itatusaidia sana kulinda afya zetu " amesema Bi Gisema
Kwa upande wake Ndg. Frank Mdimi Mkuu wa Tume ya Ushindani kanda ya ziwa ameeleza kwamba mafunzo haya yanafanyika ikiwa ni sehemu ya siku ya Maadhimisho ya ushindani duniani ambapo ofisi ya kanda ya ziwa imeamua kuja kuyafanyia katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa biashara kwa lengo la kuwajengea uwezo ikiwemo kusimamia misingi ya ushindani katika uchumi wa soko, kumlinda mlaji na kudhibiti bidhaa bandia.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga