- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
DKT. MSONDE ATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEA SEKTA YA ELIMU.
Na. Shinyanga Mc
Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI ( ELIMU ) Dkt. Charles Msonde leo tarehe 6 Oktoba, 2023 amefanya ziara ya kukagua na kutembelea Miradi ya Maendeleo hususani Sekta ya elimu Manispaa ya Shinyanga .
Akiwa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Msonde ametembelea na kukagua Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Ngokolo B, Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Shinyanga pamoja na Shule ya Sekondari Old Shinyanga,na kuongea na walimu huku akisema kuwa ameridhishwa sana na utekelezaji wa miradi hiyo na kutoa ushauri wa mambo mbalimbali ambapo ametaka mafundi kuongeza kasi ya ujenzi kwa kuzingatia viwango bora ili wanufaika waanze kutumia majengo haya.
"Niwapongeze kwa hatua mbalimbali za ujenzi uliokamilika na unaoendelea niwaombe mzingatie ubora na uimara wa majengo kwa kuzingatia thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali.
Pamoja na mambo mengine Dkt. Msonde alipata wasaa wa kuongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga na kuwasihi wasome kwa bidii ili wawezi kufikia ndoto zao kwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amekwisha waandalia mazigira bora ya kupata elimu iliyobora.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga