- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amewaonya wananchi wa kijiji cha Mwangunguli kata ya Kolandoto katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuacha tabia ya kuwasikiliza viongozi wa siasa ambao wanahujumu juhudi za Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo. Mheshimiwa Josephine Matiro ameyazungumza hayo katika kijiji hicho alipoenda kuwasikiliza maoni ya wananchi ikiwa ni mojawapo ya kituo maalumu kati ya vituo mbalimbali vilivyotengwa kusikiliza maoni ya wananchi katika juma zima la Utumishi wa Umma.
Mmoja wa wananchi Shija Luhende akieleza mbele ya mkuu wilaya kuwa maji hayafai- (Picha kwa hisani ya Marco Maduhu na Malunde Blog)
Baada ya kufika katika kijiji hicho akiwa ameambatana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa, walizungumza na wananchi wa eneo hilo ambapo hoja ya mgogoro wa mradi wa maji ya kisima kirefu katika kijiji hicho ilisikilizwa.Ilielezwa kuwa mradi huo wa maji ambao ujenzi wake ulikamilika mwaka 2014 kwa gharama ya shilingi 294.6 ulikuwa haujatumika kuhudumia wananchi kutokana na propaganda zilizokuwa zikienenezwa na viongozi wa kuanzia ngazi ya kitongoji hadi kata wakidai kuwa maji ya kisima hicho yana chumvi na hata yakitumika kupikia chakula yanakibadilisha na kuwa na rangi ya njano.
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akinywa maji yaliyoaminika kuwa hayafai kwa matumizi ya binadamu-(Picha kwa hisani ya Marco Maduhu na Malunde Blog)
Kufuatia utata huo Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Manispaa Geoffrey Ramadhan Mwangulumbi na baadhi ya wananchi waliamua kunywa maji na kuagiza chakula kipikwe kwa kutumia maji hayo ili wathibitishe kama maji hayo yana chumvi pia kama yanabadilisha chakula kuwa cha njano. Mara baada ya kunywa maji hayo, mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi na wananchi wote walithibitisha kuwa maji hayo hayana chumvi na yanafaa kwa matumizi ya binadamu.
Na mara baada ya chakula ‘wali’ kupikwa katika nyumba iliyokuwa jirani na eneo la mkutano, kililetwa mbele ya mkutano na kuwaonyesha wananchi rangi ya chakula inayoonekana baada ya kupikwa kwa kutumia maji ambayo yalitangazwa na viongozi wao kuwa yanabadilisha rangi ya chakula. Chakula kilicholetwa kilikuwa na rangi nyeupe kama ilivyo kawaida ya rangi ya chakula hicho, hali ambayo ilisababisha minong’ono miongoni mwa wananchi na baadhi ya viongozi wao wa kisiasa kuanza kuondoka wakiwa na aibu tele.
Baada ya kunywa maji na kuona chakula hakijabadilika rangi, mkuu wa Wilaya alisema kuwa amegundua kuwa viongozi wa kijiji hicho ambao ni wanasiasa wamewasababishia wananchi wao shida wakiwemo akina mama na watoto kutembea umbali mrefu wakitafuta maji na kuacha maji yaliyo karibu na makazi yao. Mara baada ya kutatua mgogoro huo, mkuu wa Wilaya aliukabidhi mradi huo kwa wananchi wa kijiji wakishirikiana na wataalam wa Manispaa.
Mkurugenzi wa Manispaa akionesha chombo kitupu mara baada ya kunywa maji ambayo yaliyokuwa yakipotoshwa na vingozi wa siasa kuwa hayafai kwa matumizi ya binadamu.(Picha kwa hisani ya Marco Maduhu na Malunde Blog)
Mwananchi wa Kijiji cha Mwamagunguli akinywa maji ya maradi uliokuwa na mgogoro kuwa maji yake yana chumvi na yanabadilisha rangi ya chakula.(Picha kwa hisani ya Marco Maduhu na Malunde Blog)
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga