- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
DC SAMIZI AONGOZA SIKU YA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA - SHINYANGA.
Na. Shinyanga Mc
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi leo Julai 25, 2023 ameongoza shughuli ya maadhimisho ya siku ya mashujaa Mkoa wa Shinyanga ambapo alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ambaye hakuwepo ambazo zilijumuisha vikosi vya ulinzi na usalama, watumishi na wananchi mbalimbali katika kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya Mashujaa katika Mnara wa Mashujaa uliopo eneo la Mazingira center.
Katika maadhimisho hayo Mhe. Samizi amewataka Watanzania kuwaenzi Mashujaa kwa kulipigania Taifa na kudumisha amani ya nchi kwani Mashujaa walitumia silaha za jadi kwa kuipigania nchi ipate uhuru .
"Nawaomba watanzania tuendelee kulipigania Taifa letu ikiwemo kudumisha amani na utulivu na historia hii ya Mashujaa ibaki vizazi kwa vizazi " alisema Mhe. Samizi.
Sanjali na hilo, Maadhimisho hayo yaliambatana na shunghuli mbalimbali ikiwemo uwekaji wa maua na silaha za asili katika mnara wa mashujaa na kufanya dua/sala kutoka kwa viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali za kuwaombea Mashujaa waliopoteza maisha na kuiombea Amani ya Nchi.
Kila ifikapo Julai 25 ya kila mwaka, Tanzania huadhimisha siku ya kuwakumbuka Mashujaa waliopoteza Maisha yao wakiutetea, Kuupigania na Kulinda Uhuru wa Tanzania.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga