- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
DC SAMIZI AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA USAFI DUNIANI MANISPAA YA SHINYANGA
Na. Shinyanga MC
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi leo tarehe 16 Septemba, 2023 ameongoza Maadhimisho ya siku ya Usafi Duniani kwa kushirikiana kufanya usafi na Watumishi kutoka Manispaa, Wafanyabiashara na Wananchi katika Soko la Kambarage.
Maadhimisho hayo ya Siku ya Usafi Duniani Mhe. Samizi amewataka wafanyabishara na wananchi kulipa swala zima la usafi wa mazingira kuwa ni kipaombele ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu katika maeneo yao ya biashara na makazi.
"Tuwe tunajijengea tabia ya kupenda kufanya usafi mara kwa mara katika mazingira yetu ili tuweze kujiepusha na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu" alisema Mhe. Samizi
Aidha, katika Maadhimisho ya Siku ya Usafi Duniani Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga imetoa vifaa vya kuhifadhia taka katika Soko la Kambarage, Mitumbani na Soko la Nguzo nane.
Maadhimisho haya ya Siku ya Usafi Duniani hufanyika kila mwaka katika mwezi Septemba kwa lengo la watu kufanya usafi katika maeneo yao mbalimbali ili kuendelea kutunza mazingira na kujiepusha na magonjwa ya mlipuko.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga