- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
DC SAMIZI AONGOZA MAADHIMISHO YA SHEREHE YA UHURU WA TANGANYIKA MANISPAA YA SHINYANGA .
Na . Shinyanga Mc
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi leo tarehe 9 Novemba, 2023 ameongoza sherehe ya maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanganyika ambapo alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa Mhe. Christina mndeme ambaye hakuwepo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali , watumishi pamoja na wanafunzi kutoka chuo cha Veta katika ukumbi wa chuo cha Ualimu shycom.
Katika Maadhimisho hayo amewataka watanzania wote kwa pamoja kuwa na mshikamano kwani , mshikamo ndio umetufanya tufike hapa tulipo, na mshikamo umeleta maendeleo kuanzia kabla ya uhuru, wakati wa uhuru mpaka tulipo hivi sasa.
" ndugu zangu tuwe na mshikamo kwani mshikamo ndio uliotufanya tukapata uhuru lakini mshikamano huo ndio uliotuletea maendelea baada ya uhuru na mpaka sasa." amesema Mhe. Samizi
Aidha, Mhe. Samizi amewataka Watanzania kutumia mitandao ya kijamii kwa manufaa mazuri ya mtu binafsi lakini pia kwa manufaa ya Taifa ili kuendelea kuleta maendeleo kwani ukuaji wa teknolojia umechangia sana kuleta maendeleo lakini pia kuharibu mmomonyoko wa maadili hivyo kuwataka watanzania kutumia maendeleo ya kiteknolojia kwa manufaa mazuri yenye tija kwa taifa letu, pamoja na kuendelea kupiga ukatili wa kijinsia unaoendelea na kuwata kutoa taarifa na sio kukaa kimya wakati vitendo vya ukatili vinaendelea.
Pamoja na mambo mengi, maadhisho haya yaliambatana na mdaharo wa mada mbalimbali zilizowasilishwa na wazee waliokuwepo kabla ya uhuru na baada ya uhuru ikiwemo mada ya maendeleo ya kiuchumi kabla ya uhuru, wakati uhuru mpaka sasa, miundombinu kipindi cha kabla ya uhuru na baada mpaka sasa.
Kila ifikapo tarehe 9 Novemba Tanzania usherekea sherehe za kupata uhuru wa Tanganyika ,ambapo Tanganyika ilipata uhuru wake tarehe 9 Novemba, 1961.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga