- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
DC SAMIZI AKABIDHI OFISI KWA DC MTATIRO
Na .Shinyanga Mc
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi leo tarehe 12 March, 2024 amemkabidhi Ofisi Mkuu wa wilaya mpya wa Shinyanga Mhe. Julius Mtatiro mara baada ya uhamisho uliofanywa na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 9 March, 2024 ambapo awali Mhe. Mtatiro alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru.
Akizungumza katika makabidhiano haya Mhe. samizi amemshuru sana Rais kwa kuendelea kumuamini na kwenda kuwatumikia wananchi wa Misungwi huku akiishukuru kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wakurugenzi kwa ushirikiano mzuri alioupata katika kutimiza majukumu mbalimbali na kumueleza Mhe. Mtatiro kuwa anamuachia Wilaya ya Shinyanga ikiwa na amani na utulivyo hivyo asiwe na wasiwasi.
“Kipekee namshuru sana Rais wetu Dkt. Samia kwa kuendelea kuniamini na kunipeleka kwenda kuwatumika wananchi wa Misungwi, niwashuru pia kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wakurugenzi kwa ushirikiano mzuri mlionipa Mhe. Mtatiro nakuachia wilaya ya Shinyanga ikiwa na amani na utulivu na usihofu utapata ushirikiano mkubwa zaidi katika majukumu mbalimbali.”amesem Mhe. Samizi
Kwa upande wake Mhe. Mtatiro amemshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu kwa kuendelea kumuamini na kumleta kuja kuwahudumia wananchi wa Wilaya ya shinyanga na kuwaomba kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wakurugenzi kumpa ushirikiano katika majukumu mbalimbali ili waweze kuwahudumia vizuri wananchi wa Shinyanga.
“Imempendeza Mhe. Rais kwa kibali cha Mwenyezi Mungu kunituma kuja kuendeleza gurudumu la maendeleo hapa shinyanga lakini pia niwashukuru kwa mapokezi mazuri mlionionesha nimefurahi namna mnavyoendelea kufanya mjukumu yenu ya kila siku kikubwa naomba ushirikiano mzuri ili tuweze kuwahudumia wananchi wetu wa shinyanga.”amesema Mhe. Mtati
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga