- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
DC SAMIZI AGAWA BLANGETI NA MAHINDI KWA WAANGA WALIOEZULIWA MAKAZI KWA MVUA KUBWA.
Na. Shinyanga Mc
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi leo tarehe 8 Novemba, 2023 amegawa blangeti na Mahindi kwa waanga walioezuliwa makazi na mvua kubwa iliyonyesha tarehe 17/10/2023 ambapo jumla ya Kaya 8 zilikosa kabisa makazi ya kuishi na kuhifadhiwa na majirani.
Akikabidhi Mahitaji hayo katika Ofisi ya Mtendaji wa kata ya Chibe Mhe. Samizi alitanguliza pole kwa waanga wote huku akitoa tahadhari ya kuwataka wajenge nyumba zenye uimara mara baada ya kipindi cha mvua kuisha ili kuepukana na maafa makubwa ya kusababisha kukosa makazi.
"Poleni sana ndugu zangu kwa maafa yaliyowapata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan anawajali na anawatambua ndo maana leo nipo hapa kwa ajili ya kuwapatia blangeti kwa ajili ya kujikinga na baridi pamoja na mahindi ya chakula lakini pia niwatake msimu wa mvua utakapopita tuboreshe nyumba zetu na tujenge nyumba zenye uimara" amesema Mhe. Samizi
Mhe. Samizi amegawa jumla ya blangeti 40 katika kaya 8 zenye watu 40 pamoja na mahindi tani 1 kwa jumla ya watu 40.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga