- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kuelekea Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanzania bara Halmashauri ya Manispaa Shinyanga kwa kushirikiana na Wakala wa misitu Tanzania TFS wamezindua kampeni ya upandaji miti katika shule ya wasichana shinyanga iliyoongozwa na mkuu wa wilaya ya shinyanga Wakili Julius Mtatiro kwa kushiriki ugawaji na upandaji wa miti kwenye kata nne za manispaa ya Shinyanga.
Awali akizindua kampeni hii ya upandaji wa miti ndani ya Manispaa ya Shinyanga Wakili Mtatiro ameelekeza Shule zote za Msingi na sekondari ndani ya Manispaa kuanzisha programu ya upandaji wa miti huku akiwataka wananchi Kuhakikisha kila Kaya wanapanda miti, lengo likiwa ni kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa upande wake Mhifadhi Misitu wilaya ya shinyanga Ndg. Fabian Balele ameeleza hatua walizochukuwa ili kupunguza uvamizi na ukataji wa miti kwenye maeneo ya hifadhi kutokana na shughuli za kibinadamu kwa kuanzisha programu ya matumizi ya mkaa mbadala.
Kwa upande wao aadhi ya wakazi wa manispaa wameeleza hali ya utunzaji wa misitu na kuziomba mamlaka zinazohusika kuendelea kutoa elimu kwa wafugaji na wakulima juu ya utunzaji wa misitu.
Kampeni hiyo ya upandaji miti ndani ya Manispaa ya Shinyanga imeanza leo kwenye kata ya nne kata ya Mwawaza, Chibe, Mwamapalala na Ndembezi ambapo zoezi hili likitarajia kuendelea kwa kata zote zilizopo ndani ya manispaa ya shinyanga, huku jumla miti milioni 1,500,000 ikitarajiwa kupanda.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga