- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro ameyataka mashirika binafsi kuendelea kushirikiana na Serikali ili kuisaidia jamii kutatua changamoto zinazo ikabili.
Wakili Mtatiro ameyasema haya leo Agosti 21,2024 wakati akizungumza na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotekeleza majukumu yake ndani ya Wilaya ya Shinyanga, katika mkutano wa mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali, kilichoketi kwa lengo la kuwasilisha taarifa za utendaji kazi na utekelezaji wa majukumu yao kwa Wilaya ya Shinyanga.
“Jamii yetu inachangamoto nyingi sana ninyi asasi za kiraia na wadau wa maendeleo tunatakiwa kushirikiana na serikali kutatua changamoto hizo katika jamii zetu Mimi nikiwa ndiye Mkuu wa Wilaya hii ambaye Mhe. Rais kaniamini niweze kumsaidia katika kipande hiki cha Wilaya ya Shinyanga nipo tayari kushirikiana na ninyi asasi za kiraia, wadau wa maendeleo Pamoja na mashirika yote kuhakikisha wananchi wanapata kile wanastahili”. amesema Wakili Mtatiro
“Niyapongeze sana mashirika yote yanayotekeleza shughuli mbalimbali za kuisaidia Serikali katika maeneo yetu,ni kweli kazi mnayoifanya ni ngumu inahitaji muda, pesa pamoja na nguvu haswa katika kizazi hiki cha kidigitali niwaombe sisi kama wadau muhimu sana tuongeze jitiada utendaji kazi ili tuweze kuisaidia jamii yetu”. ameongeza Wakili Mtatiro
Awali akisoma taarifa ya mashirika yasiyo ya kiserikali wilaya ya shinyanga Msajili Msaidizi wa Mashirika Ndg. Joram Magana amesema wilaya ya shinyanga inajumla ya mashirika 55 yaliyosajiliwa chini ya sheria na kanuni za nchi.
“kwa wilaya ya Shinyanga tunajumla ya mashirika 55 ambapo mashirika haya yanajihusisha na utoaji wa Elimu,uboreshaji wa Miundiombinu ya Maji,vyoo,utunzaji wa mazingira, kukuza Uchumi ,kusaidia Watoto wanaoishi mazingira magumu,afya, kupinga ukatili pamoja na kutoa msaada wa kisheria”.amesema Ndg. Magana
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga