- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro amewataka watendaji wote kutoka kata 17 halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wanahamasisha swala la upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi wote kwenye shule zilizopo kwenye kata zao.
Wakili Mtatiro amebainisha haya leo Novemba 12,2024 wakati akizungumza kwenye kikao cha tathmini ya Lishe kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai - Septemba 2024/2025, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga.
“Swala la upatikanaji wa Chakula kwa wanafuzi tusilichukulie kwa wepesi, walimu wanapata changamoto sana kuwafundisha wanafunzi wakiwa na njaa, kwa shule zote Manispaa ya Shinyanga ambazo zipo chini ya asilimia 100 utoaji wa chakula, Watendaji wote hakikisheni mnazungumza na wazazi umuhimu kwa wanafunzi kupata chakula wakati wa masomo”. Amesema Wakili Mtatiro.
Swala la lishe tusilichukulie tu kuwa ni Kampeni ya kitaifa wanafunzi wetu kama watapata Chakula shuleni watasoma vizuri, uzuri kwa ukanda wetu huu wa Shinyanga uhakika wa upatikanaji wa chakula upo kwa sababu wazazi wenyewe ndio tunalima. Ameongeza Wakili Mtatiro.
Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni Elimu Msingi Manispaa ya Shinyanga Mwl. Mary Maka amewasihi watendaji kutengeneza mikakati mizuri ya namna ya upatikanaji wa chakula ikiwa ni pamoja na kuwaita wazazi kwenye vikao vya shule.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga