- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius S. Mtatiro amewaasa wananchi wa mkoa wa shinyanga kutumia fursa zilizopo ndani ya nchi teknolojia na rasilimali zilizopo ndani ya nchi ili kuondokana na umaskini.
Wakili Mtatiro ameyasema haya leo Disemba 9,2024 wakati akimwakilisha mkuu wa mkoa wa shinyanga Mhe. Anamringi Macha kwenye maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara kimkoa yaliyofanyika shule ya msingi Mhangu “B” kata ya Salawe Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
“Kwa Mkoa wa Shinyanga pekee kabla ya uhuru hatukuwa na viwanda vikubwa hata kimoja lakini leo hii tunaviwanda 40 na viwanda vidogo vidogo 1,225 hivi vyote vinahitaji marighafi tunayozalisha ili viendelee kutoa bidhaa kwa wananchi kwa maslahi mapana ya uchumi wa taifa letu, hivyo niwasihi tu wananchi tutumie vizuri rasilimali tulizonazo kwa mfano Ardhi kwa ajili ya kilimo ili kujikwamua na umaskini na kuinua uchumi wa Kaya zetu”. Amesem Wakili Mtatiro
kwa upande wao wazee maarufu na wastaafu mkoa wa shinyanga Ndg. Sylvester Mpemba, Ndg. Bernard Itendele na Ndg. Zipporah Pangani wakizungumza kwa nyakati tofauti katika Maadhimisho haya wamesema kabla ya uhuru haki kuwa na hospitali badala yake walikuwa wanatumia magome ya miti na mizizi kama tiba, wali ishi kwa Neema ya Mwenyezi Mungu, wasichana hawakuruhisiwa kabisa kusoma, Mkoroni alichozingatia ni kutawala na kuwanyonya tu, kwahiyo wananchi wanatakiwa kuunga mkono jitihada za Mwl. Julias K. Nyerere na Shekhe Abeid Aman Karume kulipambania taifa hili kuwa huru.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara ni “Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji wa wananchi ni Msingi wa Maendeleo yetu” ambapo maadhimisho haya yameenda sambamba na zoezi la upimaji wa Maambukizi ya UKIMWI, uchangiaji wa Damu salama pamoja na Upandaji miti.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga